Wachumi Kukimbia Biashara ya kawaida na kufungua Jukwaa la Fedha za Kidijitali

Miaka nane iliyopita, ambapo mwanauchumi mwenye ndoto alielezea maono yake ya kutengeneza jukwaa mseto kwa ajili ya biashara ya fedha za kidijitali, wawekezaji walimcheka mbele yake. Amejitolea kwa elimu yake na taaluma kazi katika uchumi na biashara, lakini alihitaji kufanya kitu tofauti – kitu hakikuwahi kufanywa na mtu yeyote kabla.

Chris Urbanowicz, mwanzilishi mwenza na ofisa mkuu wa kitengo cha teknolojia Blockchain Board of Derivatives (BBOD), hakuruhusu wimbi la tamaa limzuie. Na kadri muda ulivyoenda, alipata washiriki wengine wachumi wenye mtizamo sawa ambao walielewa mtizamo wake. Baada ya miaka mingi ya mipango, maendeleo na utafutaji wa mtaji, Urbanowicz pamoja na timu yake wamefanikiwa kuzindua jukwaa mseto la kwanza duniani kwa ajili ya biashara ya fedha za kijiditali.

Njia mpya ya kufanya biashara ya fedha za kidijitali

Ukizungumzia njia za kufanya biashara, timu ya  BBOD haitaki biashara ya mazoea. Jukwaa linatamburisha njia mpya ya kufanya biashara: njia mseto. Haya ni maelezo mafupi tu kuhusiana na hili – Hapo zamani, wafanyabiashara wa fedha za kidijitali iliwabidi kuchagua kati ya aina mbili za masoko: soko lenye umiliki na soko huru. Aina zote zina faida na hasara, lakini machaguo kidogo yaliwaacha wafanyabiashara kufikia maamuzi magumu.

  • Soko lenye umiliki
    • Faida: mchakato wa haraka zaidi na wigo mpana kuchagua biashara
    • Hasara: urahisi wa kudukuliwa na hatari nyingine kiusalama
  • Soko huru
    • Faida: Usalama ulioimarishwa
    • Hasara: Mchakato wa taratibu na nafasi ndogo ya kuchagua biashara

Soko lipi utachagua? Utahatarisha usalama kwa kuchagua mchakato wa haraka zaidi, au utavumilia ufinyu na ucheleweshaji unaokuruhusu kuwa na udhibiti wa fedha zako? BBOD imeondoa shida hii kwa kutengeneza njia mseto, ambapo inachanganya kasi na utulivu wa soko lenye umiliki pamoja na usalama wa soko huru.

Inafanyaje kazi?

Timu ya BBOD imefanya ufumbuzi wa kipekee wa ulinzi: mfumo wa pochi zenye kuzingatia itifaki ya kompyuta. Kutumia mfumo huu, utakuruhusu kutengeneza pochi yako mahususi kwa kufanyia biashara. Kisha jukwaa litaunganisha pochi yenye itifaki ya kompyuta katika mfumo linganishi wa soko lenye umiliki wenye kasi zaidi unaotegemea teknolojia ya  GMEX Fusion, ambao huchakata miamala 1,250,000 kwa sekunde kwa wastani wa uwasilishaji wa microsecond 75. Hii inakupa udhibiti wa fedha zako wakati mfumo ukichata miamala kwa haraka. Utapata aina mbalimbali za mikataba ya moja kwa moja ndani ya jukwaa, ikiwa ni pamoja na:

  • Mkataba wa kudumu wa Ethereum-Dollar
  • Mkataba wa baadae wa Ethereum-Dollar
  • Mkataba wa baadae wa Bitcoin-Ethereum
  • Mkataba wa baadae wa Ripple-Ethereum

 

BBD tokens yenye asili yake ndani ya jukwaa, inakuruhusu kuokoa ada yenye hadi 20%. Kwa kuchanganya vipengele vyenye manufaa na ustawi wa biashara pamoja na usalama wa soko huru, Blockchain Board of Derivatives inakupunguzia hatari na kukupatia uwezo wa kuongeza faida.

Tunaifanya ndoto kuwa kweli

“Nimejawa na furaha na shukrani kwa kila mtu aliyefanya kazi na mimi kuandaa jukwaa hili la biashara,” alisema Urbanowicz. “Mwaka 2011, hakuna alieamini katika maono yangu. Na sasa watu duniani kote wanafanya biashara BBOD. Ilianza kama ndoto, na sasa imekuwa harakati za kimataifa. Tukitafakari siku za nyuma na na kuendelea mbele, timu pamoja na mimi tumejiwekea malengo binafsi ya kuendeleza jukwaa. Tunaendelea na majaribio ya mara kwamara, tunaboresha, na tunaendelea kuangalia njia mpya za kufanya vizuri kila siku. Hii ni safari yetu. Kupitia uvumbuzi wa ujasiri na uvumilivu usio na kikomo, BBOD itaendelea kukua kama jukwaa, timu na jamii.”

Mchanganyiko huu umeimarishwa na mchanganyiko wa uhifadhi huru, ustawishaji wa miamala pamoja na uchakatuaji wa kasi zaidi unakuandalia siku mpya katika ulimwengu wa biashara ya fedha za kidijitali. zaidi, uzinduzi huu unakuthibitshia kwamba kuwa na timu nzuri, maono thabiti, pamoja na kufanya kazi kwa bidii, basi kila kitu kinawezekana.

Crypto Bull

Related Articles

The cryptocurrency space is filled with opportunities, but also risks. With thousands

March 12, 2025
3 mins read
So why’s Betcoin the name on everyone’s lips? Because they’re killing it,
March 12, 2025
3 mins read

Yeshara Tokens Limited is one the companies that received the greenlight from

January 2, 2025
1 min read

As bitcoin continues to break new all-time high prices, more countries are

December 17, 2024
4 mins read
Top Reads
Editor's pick